Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa
Katika maadhimisho hayo Dkt. Kikwete ameweka ngao na mkuki katika mnara kuashiria heshima ya kumbukumbu na tukio hilo ikiwa ni pamoja na viongozi wengine kuweka silaha mbalimbali za jadi katika mnara wa kumbukumbu maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo Mizinga miwili ilipigwa kuashira amani na maombolezo na tukio hilo kuhitimishwa kwa dua iliyoongozwa na Sheikh Alhad Mussa Salumu akiwakilisha waislamu na Mchungaji John Kamoyo akiwasilisha Jumuiya ya Wakristo Tanzania pamoja na Padri Teophil Balompheti.
Hapo jana saa sita usiku uliwashwa mwenge ikiwa ni alama muhumu kwa ajili ya kumbukumbu ya mashujaa ambao walitumikia taifa kwa muda mrefu ambao wamefanya mpaka sasa Tanzania imekuwa ni nchi yenye amani.