Alhamisi , 23rd Jul , 2015

Mastaa wa muziki kutoka Uganda, Radio pamoja na Weasel wanatarajia kupiga hatua nyingine kubwa kuupeleka muziki wa Uganda katika ngazi ya kimataifa baada ya kufanikisha kolabo na msanii mkali kutoka Jamaica, Beenie Man.

mastaa wa muziki wa Uganda Radio na Weasel

Kolabo hii inakuja ikiwa ni muda umepita baada ya kaka wa kimuziki kutoka nchini humo, Jose Chameleone kufanya kolabo iliyokuwa na mchango mkubwa sana katika muziki wake na msanii huyo maarufu duniani.

Kwa mujibu wa taarifa, Audio pamoja na Video ya kazi hii inayongojewa kwa hamu tayari vimekwisha kamilika na hivi karibuni utatangazwa utaratibu wa kuachiwa kwake kwa ajili ya burudani kwa mashabiki wao.