msanii wa muziki wa bongofleva nchini Judy Entertainment
Diva huyo ameongea na eNewz kuwa yupo katika mchakato wake wa kutambulisha wimbo mpya ambao utatambulishwa siku ya Jumatano kupitia EATV akielezea kuwa utabeba ujumbe wa kupinga mauaji ya kikatili dhidi ya albino ambapo amegusia kuwa mpango mzima ni kuuzindua wimbo huo katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Aidha, Judy ametoa video yake ya kwanza kabisa ambayo anaamini kuwa itamnyanyua katika gemu ambayo ameibatiza jina Amani, wimbo uliofanyiwa kazi katika studio za BM.







