Jumatano , 17th Jun , 2015

Msanii wa muziki Amini, amejitapa kujipatia faida mara mbili kufuatia hatua yake ya kumuoa msanii

Amini

Msanii wa muziki Amini, amejitapa kujipatia faida mara mbili kufuatia hatua yake ya kumuoa msanii wa muziki na kipenzi chake cha roho Farida a.k.a Namcy Vana, kutokana na mchango mkubwa na mawazo ambayo anayapata kutoka kwa mrembo huyo kimuziki.

Amini ametolea mfano wa vile ambavyo Farida amekuwa na mchango katika kolabo ambayo wamefanya naye inayokwenda kwa jina 'Nabaki Naye', akijitapa kwa maneno yake kuwa mbali na mke, binafsi anajiona kuwa ameoa PESA pia.

Hapa Amini anaeleza mwenyewe kwa undani zaidi.

Amini na mkewe Farida (Namcy Vana)