Jumatano , 31st Jan , 2024

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema wao kama klabu walimpatia jezi namba 9 mshambuliaji wao mpya Joseph Guede lakini yeye akaomba apewe jezi namba  14 kutokana na kumkubali straika wa zamani wa Arsenal na Barcelona, Thierry Henry. 

Klabu ya Yanga ilimtambulisha  mshambuliaji wake mpya Joseph Guede aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili akitokea klabu ya Tuzlaspor inayoshiriki Ligi daraja la pili Nchini Uturuki katika dimba la Azam Complex, Chamazi kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho Azam (ASFC)

‘’Hakika tumepata mshambuliaji na tangu amekuja ana siku nne, nilienda AVIC Town kwenye mazoezi hakika hii ni mashine,’’ amesema Kamwe.