Jumanne , 25th Jul , 2023

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kucheza mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Ligi kuu ya Zambia Power Dynamo katika kilele cha Simba Day Jumapili ya Agosti 06,2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa,jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jumanne ya Leo Julai 25, 2023 Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmedy Ally amesema ni mchezo ambao watautumia katika kuwaonyesha Wanachama na Mashabiki wao kikosi chao cha kuwaletea ubingwa msimu 2023 -2024 katika mashindano ambayo wanashiriki.

'' Timu hii  ya Power Dynamo wanashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa msimu ujao hivyo  wanacheza na timu kubwa ambayo inaweza kutoa changamoto kwa wachezaji wetu”amesema Ahmedy.

kwa upande mwingine mashabiki na wanachama wa klabu hiyo  kutoka Dar es salaam wamewapongeza viongozi wao kwa kufanya usajili mzuri na wakiwataka wapenzi wa soka wajitoke kwa wingi uwanja kushuhudia wachezaji wao.

Kikosi cha Simba Sc kimeweka kambi ya wiki tatu nchini Uturuki tokea Julai 12, 2023 kwaajili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi 2023/24.