Alhamisi , 21st Mar , 2024

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Real Madrid Robinho lazima atumikie kifungo cha miaka tisa jela nchini Brazil, mahakama imetoa maamuzi hayo.

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Real Madrid Robinho lazima atumikie kifungo cha miaka tisa jela nchini Brazil, mahakama imetoa maamuzi hayo.

Robinho, 40, alikutwa na hatia na mahakama ya Italia mwaka 2017 ya makosa ya kushiriki ubakaji wa mwanamke mwenye miaka 22 raia wa Albania mwaka 2013.

Robinho amekuwa akiishi nchini Brazil, nchi ambayo haina makubaliano ya kuwakabidhi raia wake kwa mataifa mengine.

Majaji wa Brazil siku ya Jumatano waliamua kuwa mchezaji huyo atumikie adhabu yake nchini Brazil, baada ya maombi kuwasilishwa na Italy.

Atasalia kuwa huru wakati akisubiri rufaa yake dhidi ya hukumu hiyo.

Mchezaji huyo aliyeichezea Manchester City kwa miaka miwili alikiambia chombo kimoja cha habari cha Brazil siku ya Jumapili kuwa tukio hilo analotuhumiwa nalo lilifanywa kwa ‘hiari’.