Alhamisi , 4th Apr , 2024

Rais wa heshima na Mwekezaji wa klabu ya Simba SC Mohammed Dewji Maarufu 'MO' ameweka ahadi nono kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo wataweza kufuzu kwenda hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu 2023-24.

Msafara wa kikosi hicho uliohusisha watu 60 umewasili salama mjini Cairo majira ya saa 4 kamili Asubuhi huku kabla ya kuanza kwa safari hiyo,Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba SC amewaka wazi ahadi nono iliyotolewa kwa wachezaji wa klabu hiyo na Eais wa heshima wa Simba SC Mo Dewji.

''Motisha imetolewa kubwa na haijawahi kutokea kilichobakia ni wao kujitoa sisi tumeshatimiza wajibu wetu kama viongozi ''amesema Try again.

Mbali na motisha kubwa kutoka kwa Mo Dewji,Salim Abdallah maarufu kama Try Again amewatoa hofu wana simba kuelekea mchezo wa marejeano dhidi ya Al Ahly na kutamba kufanya vizuri mnamo Ijumaa ya Aprili 05-2024.

Simba itahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 2 ili kuvuka moja kwa moja kwenda nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kupoteza kwenye mchezo wa kwanza kwa kichapo cha bao 1-0 kwenye dimba la Benjamin Mkapa mnamo Machi 29-2024.