Jumatano , 6th Sep , 2023

Mafunzo ya siku mbili ya maafisa habari wa Ligi kuu NBC Tanzania na championship wapatao 28 yamefungwa rasmi Jumatano ya Leo Agosti 6, 2023 jijini Dar es salaam yakiwa na lengo kuu la kuwaongezea ujuzi na kuzifanya idara zao kwenda na teknolojia katika kuziingizia fedha klabu zao.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF na kusimamiwa na mkufunzi kutoka nchini Uganda Andwer Jackson amesema amevutiwa na muuamko mkubwa wa klabu kuleta maafisa habari huku akivutiwa na ukuaji wa soka la Tanzania .

"Amewapongeza washiriki kwa kuonesha utayari wa kutaka kufahamu mambo mapya na kupenda kujifunza kwa muda wote wa mafunzo na amewataka washiriki kuchukulia mafunzo hayo kama sehemu muhimu kwao ili kukuza mpira wetu nchini" amesema Andwer Mkufunzi.

Nao maafisa habari wa Ligi kuu na Championship ambao wameshiriki mafunzo hayo wamesema ni mazuri kwa upande wao kwani yanawapa uwezo wa kujipima wapi wapo na nini wakafanyie kazi katika klabu zao.

Maafisa Habari hao wamesema wanashukuru sana uongozi mzima wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ulio chini ya Rais Wallace Karia na Katibu Mkuu Kidao Wilfred kwa kuwezesha mafunzo hayo.