
Ni Yanga ambao wametwaa ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2022/23 hivyo KMC nao wanapiga hesabu za kufanya vizuri katika msimu ujao.
Ipo wazi kwamba kwenye mechi waliyokutana na Yanga mzunguko wa pili Uwanja wa Mkapa walishuhudia ubao ukisoma KMC 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Clement Mzize.
KMC ilipenya kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2 Mbeya City ambayo hii itashiriki Championship.
Mbeya City kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Sokoine ilipata ushindi wa mabao 2-1 na mchezo wa pili wa kumsaka mshindi ikashuhudia ubao wa Uwanja wa Uhuru ukisoma KMC 2-0 Mbeya City.
Hivyo ni rasmi kuwa KMC bado wapo ndani ya ligi na wanatarajia kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi hicho