Kocha wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Ruben Amorim kwa mujibu wa vyombo vya Habari barani Ulaya vinamtaja kuwa ndiye kocha anayetizamiwa kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag ndani ya Manchester United baada ya timu hiyo kutangaza kumfuta kazi Kocha huyo raia wa Uholanzi siku ya jana. Klabu ya Man United na Sporting Lisbon zipo kwenye majadiliano juu ya uhamisho wa Kocha huyo bora kwa sasa nchini Ureno.
Klabu ya Manchester United ya Uingereza imetangaza kumfuta kazi kocha wake Erik Ten Hag. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Ten Hag amepata taarifa ya kufutwa kwake kazi asubuhi ya leo baada ya jana kupoteza mchezo wa ligi kuu Uingereza ugenini uwanja wa London Stadium nyumbani kwa timu ya West Ham United.
Nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry amepata majeraha timu yake ikipoteza dhidi ya Los Angeles Clippers kwa alama 112-104. Curry alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi ya kikapu nchini Marekani maarufu NBA dhidi ya Clippers mchezo uliochezwa jana Jumapili Oktoba 27, uwanja wa Chase Center.
Kwa mara ya kwanza baada ya kizazi cha Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Sergio Busquets, Victor Valdes, Gerald Pique na Carles Puyol Barcelona imeanza na Wachezaji Watano kutoka kwenye kituo cha kulelea Wachezaji cha La Masia kwenye dimba la Santiago Bernabeu mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.
Usiku wa jana Oktoba 26, 2024 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu ulichezwa mchezo wa El Clasico klabu ya Real Madrid iliikaribisha klabu ya mpira wa miguu ya Barcelona katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu nchini Hispania La liga.
Mabingwa watetezi wa La Liga mara ya mwisho kupoteza mchezo wa ligi ilikuwa miezi 13 iliyopita na imecheza michezo 42 bila kupoteza, Barca inashakilia rekodi za kutokupoteza kwenye michezo 43 ya ligi iliyoanzia 2017 na 2018.Michezo mitatu iliyocheza Madrid dhidi ya Barcelona hivi karibuni kikosi cha Carlo Ancelotti kimeshinda michezo yote.
Muda mrefu Tanzania tumekuwa kwenye kilio kupata waamuzi wenye ubora wa kuchezesha michuano mikubwa ya CAF. Sasa tumeanza kuona mwanga tunapaswa kuongeza juhudi ya kuandaa Waamuzi ambao watakuwa na ubora mkubwa kuanzia kwenye ligi yetu ya ndani ambao watatuletea heshima taifa letu.
Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema ratiba ya Ligi Kuu ni ngumu kutokana na ukaribu wa michezo. Gamondi ameeleza hayo wakati mkutano na Waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Unioni hapo kesho Oktoba 26 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Kevin Durant amefunga kwenye dakika za nyongeza na kuipa ushindi timu yake ya Phoenix Suns wa Vikapu 116 dhidi ya vikapu 113 vya Los Angeles Clippers usiku wa Oktoba 23, mchezo uliochezwa uwanja wa Intuit Dome.
Kocha wa Liverpool ya Uingereza Arne Slot raia wa Uholanzi ameweka rekodi ya Kuwa Mkufunzi wa kwanza kushinda michezo 11 kati ya 12 iliyocheza mwanzoni mwa msimu na kuweke rekodi ya klabu hiyo
Klabu ya Namungo ya Ruangwa mkoani Lindi imemtangaza Juma Mgunda kuwa Kocha wao mkuu kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambaye amepangiwa majukumu mengine ndani ya klabu hiyo
Mfungaji bora wa muda wote wa NBA LeBron James usku wa jana Oktoba 22, 2024 aliweka rekodi nyingine kwenye ligi ya kikapu Marekani maarufu NBA. King aliweka rekodi ya kuchangia uwanja na mwanawe LeBron ‘Bronny’ James Jr mwenye umri wa miaka 20 kwenye mchezo uliozikutanisha LA Lakers dhidi ya Minnesota TimberWolves waliposhinda vikapu 110 kwa vikapu 103.
Nyota wa Real Madrid ya Hispania Vinicius Junior usiku wa jana Oktoba 22, 2024 aliushangaza ulimwengu wa Soka baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu. Vini alifunga magoli matatu na kuiongoza Madrid kupata ushindi wa goli 5-2.
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imemtangaza Juma Mwambusi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo David Ouma raia wa Kenya mwezi Agosti 2024. Kikosi hiko cha Wagosi wa Kaya kilikuwa chini ya Joseph Lazarao ambaye alikaimu kwa muda kipindi ambacho timu hiyo ilipokuwa inatafuta Mwalimu Mkuu.
Nahodha wa zamani wa Uruguay na Mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England atashiriki mashindano ya Tennis yatakayofanyika Uruguay Montevideo. Forlan ana umri wa miaka 45 atashirikiana na Federico Coria kwenye michezo ya wawili kwa wawili.