
Katika taarifa yake, katibu mkuu wa ZTTA Nassir Abdallah amesema, timu hiyo ilichaguliwa katika mashindano ya kombe la Muungano lililofanyika Aprili 25 mpaka 27 mwaka huu mjini Unguja.
Nassir amesema, kikosi hicho kitachuana na kikosi cha Tanzania bara ili kuwania nafasi ya kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki masahindano ya All African Games yanayotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzaville.
Nassir amesema, wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Omary Malik, Abdallah Salehe na Yusuph Mohamed kwa upande wa wanaume huku kwa upande wa wanawake ikiundwa na Mariam Abubakar, Tabia Maulid na Sabrina Yahaya.