Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkiuu wa ZFA, Khasim Salum amesema, kesi hiyo dhidi ya ZFA ambayo imeahirishwa kusomwa mpaka Februari 19 mwaka huu ipo katika mahakama kuu ambapo imefunguliwa na Ally Bakary Ally imeahirishwa kutokana na mfungua mashtaka kukataa kuwa hajafungua kesi hiyo.
Salum amesema kuwa kesi hiyo ya madai ya ubadhirifu wa fedha za kuendesha shughuli za ZFA inayowakabili viongozi wa vyama vya juu imechukua sura mpya kutokana na mfungua mashtaka kukataa na kushtaki kwa kuwa sahihi yake iliyopo mahakamani imegushiwa na suala la kufungua kesi hiyo halipo kwa upande wake.
Salum amesema, mpaka sasa wanashindwa kuendelea na shughuli zozote za kisoka kutokana na kubanwa na shughuli za mahakamani kwa ajili ya kesi hiyo ambayo mpaka sasa bado hawajajua mwisho wake.
Salum amesema, wanajua kuwa kesi zozote zinazohusiana na soka hazitakiwi kupelekwa kwenye mahakama zisizohusika na soka lakini kesi hiyo imefunguliwa na mtu anayefahamu sheria za soka hivyo kwa upande wao wanaangalia mwenendo wa kesi hiyo.
