Yanga Princes wakiwa na taji lao la ligi daraja la kwanza.
Yanga Princes ilifanikiwa kutinga fainali hiyo jana Oktoba 16, baada ya kushinda mechi ya nusu fainali kwa kuifunga Mapinduzi Queens kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kuisha kwa sare ya 1-1.
Baada ya kutwaa ubingwa huo uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu katibu Mkuu Omar Kaya umeipongeza timu hiyo kwa mafanikio chanya kwenye soka la wanawake kwa upande wa vilabu hapa nchini.
Yanga Princes sasa imepanda ligi kuu ya Wanawake Tanzania bara (Serengeti Lite Premier League) ambapo itachuana na timu zingine wakiwemo wapinzani wao Simba Queens, kuwania ubingwa wa ligi kuu soka ya wanawake Tanzania bara.


