Yanga watapaswa kujilaumu wenyewe kutokana na kukosa nafasi nyingi za kuweza kufunga mabao mengi zaidi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele. Washambuliaji kama Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa walikosa nafasi nyingi.
Chirwa ambaye ni raia wa Zambia alikosa mkwaju wa Penalti dakika ya 27 kipindi cha kwanza kufuatia kazi nzuri aliyofanya mlinzi wa kulia wa Yanga Hassan Kessy na baadae kukwatuliwa kwenye eneo la 18.

Bao pekee la Yanga katika mchezo wa leo limefungwa na nyota Juma Mahadhi ambaye alitokea benchi akichukua nafasi ya Ibrahim Ajib dakika ya 67.
Yanga itasafiri wiki mbili zijazo kwenda nchini Shelisheli kucheza mechi ya marejeano dhidi ya Saint Louis Suns United ili kupatikana kwa mshindi wa jumla atakayesonga mbele kwenye michuano hiyo. Mechi itachezwa Februari 20.


