
Yanga imelazimika kutokea nyuma ili kusawazisha bao la Prisons lililofungwa dakika ya 10 na mshambuliaji Eliuther Mpepo. Hata hivyo kabla ya kwenda mapumziko Prisons walilazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya Lambert Sabiyanka kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 35.
Baada ya Prisons kupungua Yanga ilirejea mchezoni kwa kasi na kuanza kushambulia hali iliyopelekea walinzi wa Prisons kujichanganya ambapo Jumanne EL-Fadhil alijifunga bao katika dakika ya 43.
Baada ya matokeo ya leo Yanga imebaki katika nafasi ya 3 ikiwa na alama 21 ikiachwa kwa alama 1 na Simba na Azam FC ambazo zina alama 22 zikiwa na mchezo mmoja nyumba ya Yanga.
Matokeo ya mechi zingine za leo ni ushindi wa mabao 2-1 ilioupata Singida United dhidi ya Mbeya City. Kagera Sugar imetoshana nguvu na Stand United wakitoka 0-0. Mbao FC ikiwa nyumbani imeshinda 1-0 dhidi ya Mwadui FC, wakati Ruvu Shooting wameizima Majimaji FC kwa mabao 2-1.