kikosi cha Yanga kimepangwa kundi A makundi kombe la Klabu bingwa barani Afrika ambapo kwenye kundi hili zipo pia timu za Al Hilal ya Sudani, TP Mazembe kutoka Congo DRC na Mc Algers ya Algeria
Mabingwa wa Tanzania Yanga SC wamepangwa kwenye kundi A michuano ya ligi ya ligi ya mabingwa barani Afrika, kwenye droo ya upangaji makundi iliyofanyika leo Cairo nchini Misri.
Yanga imepangwa kundi A na TP Mazembe ya Congo DRC, Al Hilal ya Sudani na MC Algers ya Algeria, Mabingwa Watetezi wa ligi kuu Tanzania bara imepangwa katika kundi ambalo lina timu mbili ambazo simeshawahi kunyakua ubingwa wa klabu bingwa Afrika TP Mazembe na MC Algers.
TP Mazembe imetwa kombe la klabu bingwa mara 5 na kombe la shirikisho mara 2 huku MC Algers ikitwaa ubingwa mara moja 1976. Timu ya Wananchi wenye makao yao makuu mtaa wa Twiga na Jangwani walitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini katika hatua ya robo fainali mashindano ya klabu bingwa Afrika msimu uliopita.
Mabingwa wa 2015 ligi ya mabingwa Afrika Mazembe ilipoteza dhidi ya Yanga kwenye michezo ya nyumbani na ugenini katika mashindano ya kombe la shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na Wananchi walifanikiwa kucheza fainali dhidi ya USM Algers ya Algeria.
Vita nyingine itakua ni kati ya Yanga dhidi ya Al Hilal, hii ni mechi ya kisasi ambapo Mabingwa wa Sudan waliiondosha katika mashindanoni timu ya Wananchi 2022-2023 mabingwa wa Tanzania wakaangukia kucheza kombe la shirikisho na kufanikiwa kufika fainali chini ya kocha Nasreedine Nabi ambaye anakinoa kikosi cha Kaizer Chief ya Afrika ya kusini.
Michezo ya makundi klabu bingwa Afrika inatizamiwa kuanza kutimua vumbi November 25/26/ 2024. Yanga inanafasi ya kuonyesha wanauwezo wa kufika mbali katika mashindano haya ya Afrika ambapo kwa msimu uliopita waliondoshwa mashindanoni kwa makosa ya Refarii kwa kukataa goli halali lililofungwa na Stephan Aziz Ki.