
Yanga inakuwa timu ya kwanza kuanza mazoezi kabla ya zote kutokana na majukumu yake ya ushiriki wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.
Yanga imeanza kujifua kwenye Uwanja wa Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam ili kujiweka vizuri kabla ya kuingia kambini.
Hata hivyo, idadi kubwa ya wachezaji haikuwa imejitokeza badala yake kulikuwa na mchanganyiko wa vijana wa kikosi cha pili ili kupata idadi itakayoonyesha ushindani.