
Meneja damu salama kanda ya Mashariki kutoka Mpango wa Damu Salama, Bwana Pendaheli Sifuel amesema kuwa wanatoa shukrani kwa viongozi wa timu hiyo huku wakizitaka klabu za Ligi kuu na vingine kuiga mfano wa mashabiki hao wa Yanga SC .
''Wamekuwa wakiunga mkono zoezi la uchangiaji wa damu kwa mashabiki wao wa Yanga kufika kwa wingi na huu umekuwa ni utamadani wao kusaidia, hii imebainisha kuwa, damu hiyo ni maalum kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali''amesema Pendaheli Sifuel.
Nao Mashabiki hao waliojitokeza katika zoezi la uchangia damu wamesema kuwa mbali na masuala ya mpira uwanjani pia wanarejesha fadhir a kwa jamii ikiwemo kufanya shuguli za uchangiaji damu na kutoa misaada kwa watoto yatima.
Kikosi cha Yanga SC kinataraji kushuka dimbani Jumamosi Julai 22, 2023 kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki wakimataifa dhidi ya Kaizer Chief ya Afrika kusini uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku kwenye kilele cha siku ya Mwananchi.