Dkt Mwakyembe ametoa kauli hiyo Bungeni katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge kilichofanyika mjini Dodoma leo (Ijumaa) ambapo alikuwa anajibu swali la muongozo wa Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobale kuhusu klabu ya Yanga kuwaachia uwanja timu ya St. Louis ya kutoka Shelisheli kufanyia mazoezi.
"Naomba nitoe rai na wito kwa wapenda mpira.Timu ya Yanga ina umri wa miaka 83 tangu kuanzishwa kwake na Simba wana miaka 82, timu zetu sasa zifike muda nazo zijenge viwanja vyao", amesema Dkt. Mwakyembe.
Kwa upande mwimgine, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson ametangaza kuhairisha shughuli za bunge leo mpaka Aprili 03 mwaka 2018 siku ya Jumanne.


