
Yanga imepanga kufanya mkutano huo Jumapili hii kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi, Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na eatv.tv Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema tofauti na Manji wamepanga kuwaandikia barua ya mwaliko viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
“Baadhi ya ajenda zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua tuliyofikia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji", amesema Mkwasa.
Alipoulizwa endapo wanampango wa kuomba kurejea kwa mwenyekiti huyo wa zamani Mkwasa alikuwa mkali na kujibu kuwa hawezi zungumzia suala hilo liko nje ya uwezo wake.