Jumatatu , 30th Oct , 2023

Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amezungumzia kuhusiana na tetesi za mshambuliaji wa klabu hiyo Moses Phiri kutakiwa na klabu ya Yanga.

"Tetesi za Moses Phiri kuondoka kwenda Yanga SC au timu nyingine niwambie tu wataendelea kumtamani kama wanavyotamani wachezaji wengine. Moses ataondoka Simba siku tukiamua kuachana nae na siku hiyo siioni, hawatampata General hata siku moja."

"Kwanza Moses Phiri anaondokaje Simba. Simba ni sehemu ya wachezaji kutimiza malengo yao, wachezaji wetu ni matajiri, wanaishi maisha ya kifalme." Amesema Ahmed Ally