
nembo ya bodi ya ligi kuu nchini .
Hapo kesho Vinara wa ligi hiyo Yanga watakuwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam kuumana na Stand United ya shinyanga.
Mwadui FC wakiongozwa na kocha wao Jamhuri Kihwelu Julio wataialika Ndanda FC ya Mtwara nayo Kagera Sugar itaendelea kusalia kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kucheza na wana kimanumanu African Sports.
Katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya baada ya kipigo kizito cha bao 4-1 kutoka kwa JKT Ruvu Tanzania Prisons watakuwa wakijiuliza mbele ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
Nayo Majimaji wakiwa na kiwewe cha kipigo kizito cha bao 5-1 kutoka kwa Toto Africans Wanalizombe Majimaji watakuwa mjini Songea kuialika Azam huku wekundu wa msimbazi Simba watakuwa na kibarua kizito watakaokuwa wageni wa wana kishamapanda Toto Africans uwanjani CCM Kitumba jijini Mwanza.
Mechi za ligi hiyo zitaendelea tena Jumapili ya Desemba 20 ambapo JKT Ruvu itaialika Coastal Union ya Tanga kwenye uwanja wa Karume nayo Mbeya City wataialika Mgambo JKT kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.