Jumanne , 18th Feb , 2025

Winga wa FC Barcelona Lamine Yamal amefikisha michezo 100 katika soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 17 akifunga mabao 21 na assist 28

Lamine Yamal - Winga wa Klabu ya Barcelona

Yamal amecheza michezo rasmi ya Mashindano 83 akiwa na klabu yake ya Barcelona pia amepata nafasi ya kucheza micheze michezo 17 akiwa na timu yake ya Taifa ya Uhispania.

Mchezo wa kwanza katika soka la kulipwa alicheza April 2023 na mchezo wake wa 100 ilikuwa ni jana katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano.

Kinda huyu anayeangaziwa kama mrithi wa gwiji wa Argentina Lionel Messi katika klabu ya Baecelona, katika michezo kumi ya mwisho aliyocheza amefanikiwa kufunga magoli manne na kutoa pasi mbili za magoli.