
Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa WUSHU Tanzania TWA Golan Kapipi amesema, timu hiyo itaundwa na jumla ya wachezaji 22 waliopatikana katika mashindano ya taifa ya vilabu na watagawanywa kwani mashindano ya nchini Poland yataanza kutimua vumbi Oktoba 13 mpaka 20 mwaka huu huku ya nchini China yakianza Oktoba 14 mpaka 20 pia.
Kapipi amesema, mashindano hayo yatashirikisha nchi zote ambazo ni wanachama wa mchezo huo na wao kama timu kutoka Tanzania wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuweza kuiwakilisha nchi vizuri katika mashindano yote.