Willian Borges Da Silva anayewaniwa na klabu ya Arsenal
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 aligomea mkataba wa miaka miwili iliyotolewa na klabu yake ya sasa ya Chelsea na huenda asiwe katika kikosi cha kocha Frank Lampard msimu ujao.
Willian Da Silva alijiunga na Chelsea msimu wa mwaka 2017 akitokea Anzi Makhachikala ya Urusi na katika michezo 339 ameifungia mabao 63 na kutwaa mataji mawili ya ligi kuu ya Enland.
Inatajwa kuwa uwepo wa Edu ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Arsenal ndio kimekua kichochezi cha kukamilisha usajili wa mbrazil mwenzake huyo kama ilivyokuwa kwa David Luiz.
Klabu ya Barcelona iliwania saini ya winga huyo msimu uliopita lakini haikufanikiwa kufuatia Chelsea kutoridhia kuondoka kwa nyota huyo.