Mshambuliaji hatari wa Leicester City Jamie Vardy akibusu kombe la ubingwa wa EPL.
Klabu ya Arsenal inaharakisha ukamilisho wa dili la usajili wa kustukiza pauni milioni 20 kwa mshambuliaji hatari wa Leicester City Jamie Vardy kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016.
Washika bunduki hao wa kaskazini mwa London Arsenal wamefikia thamani ya mauzo ya mchezaji huyo na wanamatumaini ya kukamilisha dili hiyo ndani ya masaa 24 kabla ya kikosi cha timu ya taifa ya England hakijaelekea nchini Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2016.
Katika mkataba ujao Arsenal wameahidi kumwongezea mshahara zaidi kwa juma kuliko anaolipwa sasa wa pauni elfu 80.
Jamie Vardy anatraji kueleka nchini Ufaransa kesho jumatatu akiwa tayari ni mchezaji mpya wa Arsenal baaada ya kukamilisha uhamisho huo wa pauni milioni 20 kutoka Leicester City.
Ni wiki chache tu zimepita tangu aipe ubingwa wa kustukiza wa Ligi Kuu ya England timu ya Leicester mshambuliaji huyo ataelekea Arsenal hii leo jumapili kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba.
Uamisho huo unamfanya kocha wa Leicester Claudio Ranieri, akiri kutoweza kuzuia nyota wa kikosi chake wasinyakuliwe na vilabu vikubwa barani Ulaya.
Vardy, ambaye alisaini mkataba mpya na timu hiyo miezi minne iliyopita ukiwa na kipengele cha kuuzwa bado anafuraha kuwepo ndani ya Leicester lakini akathibitisha kuwa tarehe 29 Mei ilikuwa ni nafasi yake ya pekee kujiunga na moja ya timu kubwa nchini humo.
Arsene Wenger amefanya uamuzi wa kustukiza katika usajili wa Vardy baada ya vilabu vingi vikubwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo.
Kwa sababu kocha mkuu wa England Roy Hodgson ataki wachezaji wa kikosi chake wafikirie usajili wao wakati wa michuano ya Euro au kufanya vipimo vya afya ndio maana kocha wa Arsenal ametaka dili hiyo ikamilishwe haraka kabla ya timu hiyo kuondoka kwenda Ufaransa kesho Jumatatu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.