Taarifa WBA imesema hakukuwa na ushahidi wa kutosha ili kubatilisha uamuzi wa awali huku kesi hiyo ilipelekwa kwenye kamati maalumu ya waamuzi na kujiridhisha kuwa Dubois alimdondosha Usyk kupitia ngumi iliyopigwa chini ya mkanda ambapo ni kinyume na sheria za ngumi duniani.
Oleksandr Usyk anayeshikilia mikanda ya WBA,IBF na WBO alidondoshwa kwenye ulingo kwenye mzunguko 5 na kupewa dakika 4 za kukaa sawa kabla Dubois kuchapwa kwenye mzunguko wa 9 na kuitetea mikanda yake anayoishikilia kwa sasa.