
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akitoka Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara.
Waziri Kangi Lugola amefikia hatua hiyo baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya kumweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka watuhumiwa hao mahabusu.
''Tabia hii siku zote tunaipinga imekuwa ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio maana nimekuja ghafla, OCS umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, sasa na wewe unaingia ndani'', amesema Kangi wakati akimweka ndani OCS Ibrahim Mhando.
Mkuu huyo wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, alishindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects.
Mbali na hilo Waziri Kangi pia amemhoji Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas Theophilius Kessy, ambaye ndiye kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara chini ya kiwango.