Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga-Ibrahimu Akilimali
Baraza la wazee la klabu ya Yanga ya jijini DSM, umeelezea kusikitishwa kwake na kitendo cha baadhi ya wanachama waonapinga maamuzi halali ya mkutano mkuu ya kuwaongezea muda viongozi wa sasa wa klabu hiyo.
Akiongea kwa niaba ya wazee wenzake, katibu wa baraza hilo mzee Ibrahim Akilimali amesema kimsingi mkutano mkuu wa June Mosi mwaka huu ulifanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya klabu hiyo hivyo wale wote wanaoyapinga maamuzi hayo hawaitakii mema klabu hiyo.
