Jumatano , 6th Apr , 2022

Kocha wa mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, Pablo Franco ameanza kupiga hesabu mapema juu ya kuziba pengo la beki wake wa kati Joash Onyango ambaye atakosekana kwenye mchezo wa robo fainali unaotarajia kuchezwa Aprili 17 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Sadio Kanoute

Simba imepangiwa kucheza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na iwapo itapita hatua hiyo na kutinga nusu fainali watacheza dhidi ya mshindi wa mechi ya Al Ahli Tripoli dhidi ya Al-Ittihad Club zote kutoka Libya

Kwenye hatua ya robo fainali, Simba ambayo itaanzia nyumbani itamkosa Onyango ambaye ana kadi tatu za njano alizoonyeshwa katika mechi za makundi.

Onyango amepata kadi za njano kwenye mechi dhidi ya US Gendermerie Nationale 1-1, Berkane 2-0 Simba na tena dhidi ya Simba 4-0 US Gendermerie.

Kukosekana kwa Onyango kutampa nafasi Kennedy Juma kuingia kikosini kutokana na ubora wake na hivyo kumpunzia mzigo kocha Franco iwapo atamshawishi kocha wake. 

Kanoute alipata kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya Berkane na mechi zote mbili za US Gendermarie hivyo atakosekana kwenye mchezo ujao.