Jumanne , 6th Mei , 2025

Uhondo wa ligi kuu ya wanawake Tanzania Bara utarejea tena Jumatano hii  Mei 7 ,2025 ambapo  vinara wa ligi hiyo  JKT Queens watakuwa nyumbani Meja Isamhuyo kuwakaribisha Simba Queens mabingwa watetezi wa michuano hiyo. 

JKT Queens vs Simba Queens

Mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 10 jioni una nafasi kubwa  ya kuamua ubingwa wa ligi ya Wanawake   msimu huu wa 2024-2025 ikiwa imesalia michezo 4 ligi hiyo  kutamatika .

JKT Queens  wanaongoza ligi kwa alama 38 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 14 idadi sawa na Simba Queens anayeshika nafasi ya pili akiwa na alama 37

Mchezo wa mzunguko  wa kwanza uliowakutanisha wababe hao wa ligi ya wanawake ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 ,Simba Queens walitangulia kwa  bao la Elizabeth Wambui na baadae Donisia Minja akawasawazishia JKT Queens.