
Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Chama cha Mpira wa Wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA Nassoro Shariff amesema, maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yameshakamilika ambapo vilabu vyote vimeshapata ratiba ili kuanza maandalizi mapema.
Shariff amesema baada ya mashindano hayo Februari mwaka huu watakuwa na mashindano mengine kwa upande wa timu za wanawake.