Kocha, Jamhuri Kihwelo 'Julio'
Julio ameyasema hayo alipozungumza na www.eatv.tv kuhusiana na kiwango pamoja na matarajio ya Taifa Stars baada ya ushindi dhidi ya Cape Verde katika uwanja wa taifa.
“Baada ya kufungwa goli tatu, watu wengi walikata tamaa na wengine wakaanza kuibeza timu kwa maneno machafu lakini mimi nilisema watanzania wengi mpira hawajui, ndomana unakuta wanakimbilia timu nyingi za EPL na huko utasikia Mourinho hajui, kocha fulani kakosea”, amesema.
“Lakini katika mtazamo, mtu aliyekuwa profesa wa mpira anawezaje kukosea na mimi nilisema baada ya kupoteza bao tatu kule kuwa wametufunga, wametupita lakini na sisi tutawapiga na kuwapita nyumbani kwetu”, ameongeza.
Pia kocha huyo ambaye aliwahi kuifundisha Simba, amesema kuwa tatizo ambalo lilipelekea Taifa Stars kufungwa Ugenini katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Cape Verde ni kutokana kujiamini kwa wachezaji kupitiliza.
“Tatizo ni kwamba sisi tulivyokwenda kule tulikuwa ‘Over confidence’ (kujiamini kupitiliza), sisi sasahivi timu yetu tumepatiwa kitu kimoja, ni kama mtu ambaye huna pesa halafu umepata pesa ya haraka, unaweza kuwa na munkari ya kununua gari, nyumba, vile na vile. Sasahivi tuna wachezaji wa Kimataifa kama nane, ile kidogo ilitupa kichwa kuwa wingi wetu utatubeba”.


