Ijumaa , 4th Apr , 2014

Watanzania watano wamefanya mtihani wa uwakala wa wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), ulifanyika jana (Aprili 3 mwaka huu) duniani kote.

Watahiniwa wote hao walifanya mtihani huo ambao ulikuwa na maswali kutoka FIFA na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na baadae watatumiwa majibu yao kupitia TFF

Ambapo afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa majibu ya kufaulu kwa mtihani sio kigezo pekee cha mtahiniwa kupata leseni hiyo bali kuna mambo mawili ya kuzingatia kama maagizo ya FIFA ikiwemo suala la kuwa na kava ya leseni na kiapo cha kisheria.