Jumatatu , 17th Oct , 2016

Mwanariadha wa Kenya, Daniel Wanjiru, ameshinda katika muda bora wa mashindano ya arobaini ya TCS Amsterdam Marathon nchini Uholanzi.

Wanjiru, alitumia muda wa 2:05.21 na kuivuka rekodi ya mshindi mara tatu, wa Amsterdam Marathon, Wilson Chebet ya masaa 2:05.36 mwaka 2013.

Wanjiru alifuatiwa na Wakenya wenzake, Sammy Kitwara, aliyetumia masaa 2;05.45, na Marius Kimutai, aliyetumia masaa 2:05.47.