Jumatatu , 4th Apr , 2022

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za wizi wa vyuma kwenye daraja la Tanzanite jijini Dar es salaam.

Askari Polisi akiwadhibiti watuhumiwa na kuwaingiza kwenye gari la Polisi

Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amefafanua kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakijaribu kufungua baadhi ya vyuma vilivyotumika kama ngazi kwenye utengenezaji wa daraja hilo.

Tazama Video hapo chini