Jumatano , 29th Aug , 2018

Wachezaji, wakufunzi na wafanyakazi wengine wa Manchester United wanaamini Jose Mourinho atafutwa kazi iwapo atashindwa mechi nyingine moja.

Kocha Jose Mourinho kwenye moja ya mechi za Manchester United.

Maafisa wakuu wa klabu hiyo hata hivyo bado wana imani kwamba Mourinho, 55, kuwa anaweza kubadilisha mambo katika klabu hiyo hata baada ya United kushindwa mechi mbili kati ya tatu za kwanza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza tangu 1992-93.

Beki wa zamani wa Manchester United Paul Parker, 54, anasema meneja wa sasa wa klabu hiyo Jose Mourinho anafaa kuihama klabu hiyo baada yao kushindwa 3-0 na Tottenham nyumbani Jumatatu.

Lakini wakati hayo yakiendelea inadaiwa kuwa kumbe Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho, alitaka kumnunua mchezaji aliemtika katika majanga yanayoendelea sasa, Mbrazil, Lucas Moura, wa Spurs kwa mujibu wa wakala wa Mchezaji huo.

Wakati Mourihno akilia na safu yake ya Ulinzi, Beki wa kati ambae ameshwahi kuichezea Manchester United ambae kwa sasa anakipiga na Barcelona Gerard Pique, 31, amesema hawezi kamwe kurejea Manchester United, Mhispania huyo aliondoka Old Trafford na kuhamia Nou Camp mwaka 2008.