Jumatano , 22nd Jun , 2016

Wadau na michezo nchini Tanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa ngumi nchini.

Mmoja wa waandaaji wa mapambano nchini Dotto Texas amesema, wadau wa michezo wanatakiwa kuangalia michezo mbalimbali na sio kw aupand wa soka peke yake ili kuhakikisha vijana ia wanapata ajira kupitia michezo.

Texas amesema, mchezo a ngumi umekuwa ni kazi kama zilivyo nyingine na hata watakaposaidiwa watakuwa na uwezo wa kuweza kuitangaza nchi katika ramani ya michezo.