
Afisa Habari wa Azam FC Jafari Maganga amesema, wachezaji hao ambao ni Allan Wanga, Jean-Baptiste Mugiraneza na Didier Kavumbagu watawasili hii leo kwa ajili ya mazoezi ya mechi ya Ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons Jumamosi ya wiki hii.
Maganga amesema, wachezaji wa ndani waliokuwa kambi ya timu ya Taifa wamesharipoiti kambini ambapo kesho wataanza mazoezi ya pamoja ambapo kocha atakuwa na mazoezi kwa ajili kuwaweka sawa kwa ajili ya kupambana na ligi ambayo kwa msimu huu ni ngumu kutokana na kuwa na bingwa mmoja bila ya kuwa na mshindi wa pili hivyo kikosi kinafanya maandalizi ili kuweza kupambana.