Akizungumza na East Africa Radio, Kassim amesema watoto hao wamezidi kuonesha vipaji lakini ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika Mashariki wanatakiwa kuanza maandalizi mapema.
Kwa upande wake, mmoja wa wachezaji wa mchezo huo, Gloria Lyimo amesema michuano hiyo imekuwa na changamoto nyingi suala linalompelekea kuendelea kufanya vizuri kutokana na kila mchezaji kuhitaji kushinda katika kila mchezo.