Jumatatu , 3rd Nov , 2014

Wachezaji wa timu mbalimbali zinazoshiriki michuano ya ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam RBA wametakiwa kufuata sheria za mchezo huo na kuacha kuwatupia lawama waamuzi wa michuano hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, mmoja wa muamuzi katika michuano hiyo, Gozbert Boniface amesema kila timu inahitaji ushindi, hivyo wanaposhindwa wanahisi kama wameonewa suala ambalo sio la kweli.

Boniface amesema hivi sasa kunasheria mpya ambazo zimeshaanza kusambazwa kwa vilabu vyote vya mpira wa kikapu ambapo wanatakiwa kuzisoma na kuelewa kwa makini ili kuweza kuujua mchezo huo pamoja na sheria zake