Jumatano , 29th Jul , 2015

Mabingwa wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara wanatarajia kushuka dimbani leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ngugu zao ambao ni makamu bingwa Azam Fc katika robo fainali ya pili ya michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Kombe la Kaga

Mchezo huo utatanguliwa na mechi ya KCCA ya Uganda ikicheza dhidi ya Al Shandy ya Sudan ambapo atakayeibuka na ushindi katika mchezo huo atakutana na Yanga au Azam Fc katika hatua ya nusu Fainali itakayopigwa siku ya Ijumaa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika robo fainali iliyomalizika hapo jana, Gor Mahia iliichapa Malakia mabao 2-1 huku Al Kharthoum ya Sudan ikiitoa APR kwa kuichapa mabao 3-0 na kupelekea Gor Mahia kukutana na Al Kharthoum katika hatua ya nusu Fainali mchezo utakaochezwa siku ya Ijumaa.