Nyota wa Real Madrid ya Hispania Vinicius Junior usiku wa jana Oktoba 22, 2024 aliushangaza ulimwengu wa Soka baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu. Vini alifunga magoli matatu na kuiongoza Madrid kupata ushindi wa goli 5-2.

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema anauhakika kuwa mchezaji wake Vinicius Jr atashinda tuzo ya Ballon d’Or zitakazotolewa Jumatatu ya Oktoba 28 huko Paris Ufaransa. Akiamini kiwango alichokionesha Mchezaji wake siku ya jana kitachochea kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2024.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga hat-trick ya kuvutia dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa jana na kusaidia timu yake iliyokuwa nyuma kwa magoli 2-0 na kuonekana kama ingepoteza mchezo huo dhidi ya Mabingwa kombe la Klabu bingwa barani Ulaya wa msimu wa 1996-1997 Dortmund kwa kushinda 5-2 Santiago Bernabeu.
Mashabiki wa Real Madrid waliliimba jina Vinicius Jr kuwa atashinda tuzo hiyo kubwa ulimwenguni na baada ya mechi Carlo Ancelotti alimwita Vinicius Jr na kusisitiza kuwa atashinda Ballon d'Or kutokana na ubora aliouonesha msimu uliopita.
Kwa upande wake mshambuliaji huyo wa Brazil alipoulizwa kuhusu kushinda tuzo hiyo alijibu kwamba malengo yake ni kusalia Real Madrid na kuendelea kuweka historia ndani ya klabu hiyo mabingwa mara 15 wa UCL. Mara ya mwisho Mchezaji kutoka Brazil kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ilikuwa msimu wa 2006-2007 Ricardo Eziksen Leite 'Kaka' alishinda tuzo hiyo mbele ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.