Jumapili , 12th Jun , 2016

Kuelekea katika ufunguzi wa dirisha la usajili, vilabu vya Ligi Kuu Tanzania Bara vimeshauriwa kuwa na utulivu ili kuweza kusajili wachezaji watakaokuwa na manufaa kwa timu.

Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Stand United Muhibu Kanu amesema, timu inapokuwa na amani na utulivu huwa inafanya usajili ambao huwa na maana na mwisho wa siku huwa na wachezaji wa muda mrefu katika timu.

Kanu amesema, timu zinatakiwa kufanya usajili wa kiufundi zaidi na wa kitaalamu ili mwisho wa siku wasije wakajialaumu.

Kanu amesema, kwa upande wa timu yake wamejipanga vizuri kwa ajili ya usajili kwani wanaangalia na kufanya marekebisho kuanzia upande wa kocha, benchi la ufundi na hata wachezaji kwa ujumla.

Dirisha la usajili usajili Ligi Tanzania Bara linatarajiwa kufunguliwa Juni 15 mwaka huu kwa vilabu vyote shiriki.