Alhamisi , 14th Jan , 2016

Miamba ya soka nchini Uhispania Real Madrid na Atletico Madrid wamepigwa marufuku kutonunua wachezaji wapya sokoni kwa vipindi viwili.

Nembo za vigogo vya soka nchini Hispania Atletico madrid (kulia)na Real Madrid(kushoto)

Klabu hizo zimeadhibiwa na shirikisho la soka duniani FIFA kwa kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji ambao bado ni watoto.

Marufuku hiyo haitaathiri kipindi cha sasa cha kununua wachezaji, ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu huku wakitarajiwa kutosajili katika kipindi cha dirisha la Julai hadi Agosti mwaka huu na Januari 2017.

Atletico pia wametozwa faini franka 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 622,000 za Uingereza, nao Real wakatakiwa kulipa franka 360,000 (£249,000).