Jumatatu , 20th Jun , 2016

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema anaamini kuwa mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy hataitaka Arsenal hivyo ataendelea kubaki Leicester City katika msimu ujao.

Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy

Alizungumza hayo baada mmiliki wa klabu ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha kusema kuwa Vardy atabaki na mabingwa hao wa Uingereza katika msimu ujao.

Hata hivyo chezaji huyo alipouliza alikataa kueleza atacheza wapi msimu ujao na kusema kuwa kwa sasa anafikiria michuano ya Euro na siyo kitu kingine.

Wenger alipoulizwa kuhusu kumleta Vardy uingereza alisema: "Hapana Jamie Vardy yuko Leicester kwa sasa hivi na kwa ninavyojua mimi, Jamie Vardy atabaki Leicester msimu ujao.

Vardy aliwekwa Benchi kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Russia ila aliweza kujipatia goli alipotokea benchi kwenye mechi ya pili dhidi ya Wales.