Taarifa ya Simba SC kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba imeeleza kuwa Uwayezu mwenye uzoefu wa miaka 10 ataanza rasmi majukumu yake ndani ya Simba SC mnamo Agosti Mosi-2024 huku Uongozi wa Simba SC umesema una imani kubwa na Regis kwenye kuendeleza kasi ya mafanikio ndani ya timu hiyo.
Uwayezu Regis amewahi kufanya kazi ndani ya Shirikisho la Mpira na Nchini Rwanda (FERWAFA) pamoja na kuhudumu nafasi ya Makamu wa Rais wa Klabu ya APR FC ya Rwanda.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Simba kuwa na CEO kutoka nje ya nchi, kwani awali iliwahi kumuajiri, Senzo Mbatha kutoka Afrika Kusini ambaye aliondoka kutua Yanga kabla ya kurithiwa na Mzambia, Andre Mtine aliyetokea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.