Jumanne , 7th Jun , 2022

Kiungo wa zamani wa Liverpool na England Danny Murphy amesema iwapo angekuwa kwenye sehemu ya uongozi wa klabu ya Manchester United basi angependekeza nafasi hiyo kupewa kocha mkuu wa England Gareth Southgate badala ya kocha wa sasa Erik Ten Hag.

(Kocha mkuu wa England Gareth Southgate na Msaidizi wake Steve Holland wakiwa mazoezini)

Murphy mwenye umri wa miaka 45 amewapigia chapuo kocha mkuu wa England Gareth Southgate na msaidizi wake Steve Holland kama machaguo sahihi kuliko mkufunzi wa sasa Erik Ten Hag na msaidizi wa Steve McClaren

'nawajua Gareth na Steve kwa muda mrefu ,nafikiri wametoka mbali sana kwa pamoja na wanafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na umeonesha matunda kwa kiasi kikubwa .Mafanikio waliyoyapata na England,kuweza kuwasimamia wachezaji wenye majina makubwa na Southgate ameweza  kuhusika  kutengeneza vipaji vizuri kwenye soka “amesema Murphy

Ten Hag amejiunga na United akitokea klabu ya Ajax Amsterdam aliyoiongoza kutwaa mataji matatu mfululizo ya ubingwa wa ligi kuu nchini Uholanzi maarufu kama Eredivisie huku tayari akiwa anajiandaa na msimu mpya ndani ya mashetani wekundu wa Old Trafford .