Kamishna Suleiman Kova akiongea na Waandishi wa habari
Katika kuhitimisha ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza kuimarisha Ulinzi katika mchezo kati ya Simba na Dar es salaam Young Africans maarufu kama Yanga Mchezo utakaopigwa siku ya Jumamosi katka uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia namna jeshi hilo lilivyojipanga kukabiliana na uhalifu katika mchezo huo,Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema kuwa wameshirikiana na Shirikisho la Kandanda nchini pamoja na Uongozi wa uwanja kuhakikisha mchezo huo unamalizika salama.
Aidha, Kamishna kova amesema wameweka kila aina ya ulinzi kujihadhari na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwabaini wanaopanga kufanya matukio ya kigaidi katika mchezo huo.